Neema Mbise ni jina ambalo lipo
kwa wingi vinywani na masikioni mwa watu wengi hapa nchini Tanzania na hasa
katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, nan chi jirani ya Kenya, hii ni kutokana
na huduma yake ya uimbaji wa nyimbo za
Injili. Sauti ya kanisa wiki hii ilipata nafasi ya kuzungumza na mtumishi huyo
wa Mungu kuhusiana na huduma yake ya uimbaji
Sauti ya kanisa ilitamani kujua
zaidi siri ya mafanikio ya huduma yake ya uimbaji, Neema Mbise alisema,
hakutarajia kuwa siku moja atakuwa muimbaji wa nyimbo za Injili, kwakuwa ndani
mwake aliwaza kusoma zaidi na kufanya mambo mengine yanayohusu familia yake,
lakini akiwa katikati ya masomo yake,
ndipo alipokutana na Mungu na kwa njia ya kuokolewa, baada ya hapo ndipo
aliposikia sauti ya Mungu ndani mwake mara kwa mara ikimwambia Neema nitumikie,
na hakujua kipi afanye ili kuendane na kile anacho kisikia ndani mwake, kwahiyo
mara nyingi akawa anajaribu kufanya majukumu mengi katika kanisa alilokuwa
anaabudu, kama kufanya usafi na kuwakaribisha watu kanisa, lakini bado ile
sauti ilizidi kusema ndani mwake kuwa nitumikie, ndipo alipoanza kuomba kwa
lengo la kuuliza kwa Mungu juu ya sauti na wito anaousikia juu ya utumishi
Ndipo alipopewa jibu kuwa nataka
unitumikie kwa njia ya uimbaji, alishangaa na kuona ni jambo ambalo ni zito
kwake, kwakuwa alianza kuwaza nijinsi atakavyo weza kutunga nyimbo, na tena
nijinsi gani nitakavyo weza kusimama mbele ya watu na kuimba, alipata wakati
mgumu wa kuwaza mambo mengi yanayofanana na hayo, nilikuwa ni mwepesi kuona
aibu mbele za watu wengi, na hasa katika makusanyiko ya kanisani, lakini kwa
kuwa alikuwa amejifunza kupitia kwa watumishi wa Mungu waliokuwa wanafundisha
kanisa, juu ya jinsi ya kumtumaini Mungu, naye alizidi kusema moyoni mwake,
Mungu nakutegemea na kukutumaini wewe
Neema Mbise anasema, anamtumikia
Mungu kwa makusudi ya kuwafanya watu wote wamjue Mungu na kuokolewa, namtumikia
Mungu kwakuwa ni agizo lake ndani mwangu, na wito niliopewa, kwahiyo namtumikia
Yesu si kwa lengo la kutafuta faida hapa dunia, kama kupata mauzo au mapato
makubwa kutokana na huduma yangu ya uimbaji la, lengo langu nililopewa ni
kuhubiri Injili kwa njia hii ya uimbaji.
Wakati Mungu alipokuwa anaweka
agizo lake ndani mwangu, aliniambia matokeo yatakayo ambatana na huduma yangu
ya uimbaji, na moja kati ya vitu ambavyo nimeanza kuviona, ni uponyaji wa
wagonjwa kupitia huduma yangu ya uimbaji, mara kadhaa watu wameshuhudia kwamba,
wakati naimba walipokea uponyaji au imani yao kiroho kuinuliwa baada ya kukata tamaa
kwa muda mrefu, kwahiyo kupitia huduma yangu ya uimbaji watu wamekuwa
wakifunguliwa kutoka katika vifungo vya magonjwa nk
Wito wa mtumishi huyu wa Mungu kwa
wakristo na watanzania wote nikwamba, kwakuwa wengi wameona huduma yake, yeye
anaomba maombi ya watu wote ili azidi kumtumikia Mungu kwa viwango vya usafi kiroho
na utakatifu, pia anapenda kusikia ushauri kwakuwa anaamini ni njia ambayo
Mungu utumia kuikuza huduma yake. Na alitoa wito kwa waimbaji wa nyimbo za
Injili, kwamba tunapaswa kuwa kioo cha kanisa kwa kuwa huduma ya uimbaji ni
huduma inayoonekana kwa macho tofauti na huduma ya mwana maombi, nawaomba tuwe
na sifa njema na maisha yenye ushuhuda na tupendane kwakuwa sote ni wamoja
katika huduma moja
Sauti ya kanisa ilifanikiwa
kupata namba yake simu ambayo uitumia katika huduma ya uimbaji, nayo ni
0655-234449, pia yupo katika mtandao wa facebook kwa anuani ya mbisseneema,
kwasasa yupo katika matengenezo ya website yake kwaajili ya huduma yake ya
uimbaji, website atakayo itumia kwaajili ya kuinua waimbaji mbalimbali.
Sauti ya kanisa itaendelea
kukuletea habari zinazo husiana na Neema Mbise, pamoja na waimbaji wengine wa
ndani na nje ya Tanzania