Nikisoma maandiko matakatifu ya mwana wa Mungu Yesu ninaona mara kwa mara akizungumzia na kusisitiza sana kuhusu umoja kwa watu wote, na akiwataka wawe na umoja kama yeye alivyo na umoja na Mungu baba, kwahiyo umoja ni tabia ya Mungu na agizo la Mungu
Nilichogundua katika pita pita zangu ndani ya uwanja huu wa sauti ya kanisa ni kwamba, vyama vya siasa hapa nchini kwa sehemu kubwa vinafanya kazi ya Mungu kwa sehemu kubwa pale wanapowajenga watu wao kuwa na umoja, kwa mfano angalia katika matukio ya picha hizi za viongozi wa chama cha mapinduzi, CCM,
HAPA NI KATIBU MWENEZI AKIWA NA WANACHAMA NA WANANCHI HUKO MKOANI MOROGORO, WAMEKUSANYIKA KWA UMOJA KUPITIA CHAMA CHAO
KATIBU MKUU WA CCM. MHESHIMIWA KINANA, NAYEYE YUPO NA WANANCHI WA ULANGA MKOANI MOROGORO, NI KAMA ANAWAMBIA HIVI:- TUSHIKAMANE NA TUWE NA UMOJA, NA UENDA ANAYASEMA HAYO KWA MAANA YA UMOJA NI NGUVU
PICHA ZA MWANZO KULE JUU, WALIKUWA NI WANANCHI NA KIONGOZI MMOJA MMOJA KWA UMOJA, SASA HAPA WAMESIMAMA VIONGOZI MBELE YA JUKWAA KWA PAMOJA, WAKISEMA NA SISI PIA NI WAMOJA!!!
Huo ni ujumbe wangu kwako, naomba uutafakali na kuulinganisha na maneno au mafundisho aliyokuwa akiyafundisha Bwana Yesu alipokuwa hapa Duniani, kama utagundua mapungufu, basi ni katika hali ya uanadmu tu
Jumanne, 16 Aprili 2013
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595
0 comments:
Chapisha Maoni