Wakenya wamempata Rais mpya ambaye ni Mh Uhuru Kenyatta,
ameapishwa kulingana na katiba ya Kenya, na umati mkubwa wa watu walikuwa
wanashuhudia, miongoni mwa watu waliokuwepo ni wakuu wa nchi mbalimbali,
mawaziri wakuu na mabalozi nk, kwa hakika ni jambo la kumshukuru sana Mungu kwa
hatua ya kumpata kiongozi mkuu wa nchi, wajibu wa wanakenya ni kumwombea kwa
mwenyezi Mungu ili makusudi ya kuchaguliwa kwake yaweze kutimia, tunaamini
kwamba amani itatawala nchini Kenya, na maendeleo yatapatikana, tunaomba
pasiwepo na matengano kati ya wanakenya, upendo na umoja uendelee na kudumishwa
Kenya, Mungu ibariki Kenya na Mungu ibariki Africa
0 comments:
Chapisha Maoni