katika mahubiri ibadani hapo, mchungaji huyo alisema, Kanisa nyakati hizi tulizo nazo
leo, limetiwa unajisi, nyakati zile za Yesu palikuwepo na mwanamke mmoja ambaye
alikuwa na tatizo la kutokwa na damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, kwa
nyakati zile yule mwanamke alikuwa ni najisi sana, na watu walikuwa
wakijiepusha kuwa naye karibu, kwahiyo alitengwa na watu kila alipokwenda.
Lakini siku moja alisikia habari za Yesu, na akachukua hatua ya kwenda kwa Yesu
akisema moyoni mwake, nikigusa vazi lake nitapona.
Jinsi alivyokuwa yule mwanamke
katika hali ya unajisi wake, ndivyo lilivyo kanisa la leo, kanisa limejaa
unajisi, wahubiri na wachungaji wanaofanya maombezi kwa kuwatoza watu pesa,
maombezi hayo ni batili “nifeki” hao ni matapeli wakawaida. Waimbaji wa nyimbo
za Injili wanaotoa huduma kwa kuomba malipo ya ile huduma hao pia ni matapeli
wakubwa na aibu yao inakuja
Matendo hayo ndiyo yamelitia
kanisa unajisa na kanisa linanuka! Na katika ulimwengu wa roho kanisa linavyo
onekana mbele za Mungu ni wakati ule yule mwanamke aliyetokwa damu alivyokuwa
akitengwa na wanadamu kutokana na unajisi aliokuwa nao, ndivyo na kanisa la
sasa linavyo tengwa na Mungu kutokana na unajisi huu.
Mchungaji aliwataka waumini wa
kanisa la Bethel Assemblies Of God watubu kwaniaba ya kanisa la Tanzania ili Mungu
alitakasa kanisa kwa kuliponya na kuondoa unajisi
0 comments:
Chapisha Maoni