Wananchi wamejitokeza katika sehemu nyingi za Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha kiongozi wao Nelson Mandela Mandela.
Mji wa Johannesburg umemiminika watu
waliojitokeza kumkumbuka Mandela na kutoa rambi rambi zao kwa jamii,
familia na marafiki wao.Viongozi duniani pia wameendelea kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha Mandela.
Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo jana Alhamisi saa za usiku naye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyesema kuwa Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama mtoto wao , baba yao na kiongozi wa taifa hilo.
Mandela alifariki nyumbani kwake mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa Mzee Mandela, miongoni mwa wengine kama Oliver Tambo, Govan Mbeki na wengine, walijitolea maisha yao na ujana wao wote katika kupigania haki na kuikomboa Afrika Kusini. Walijivunia kweli walichoamini na wakatekeleza. Sasa ni jukumu letu na wadogo wetu kuendeleza kazi ya Mandela.''
Rais wa Malawi Joyce Banda, "Wakati kama huu, sote tumepata mshtuko. Sio kuwa hatukujua kitatokea, lakini ni huzuni kwa tulichopoteza. Ningependa kuelezea masikitiko yangu kwa kumpoteza kijana wa Afrika Dr. Nelson Mandela kwasababu vita alivyopigana sio tu dhidi ya ubaguzi wa rangi bali ni vita dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote dhidi ya binadamu.
Na ndio maana vijana, na wazee, wake kwa waume, weupe na weusi tajiri na masikini wote wamejihusisha na yeye na vitu alivyopigania."
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.
Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, "Kifo cha mandela. Huyu alikuwa mwakilishi wa utu duniani.
Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa wengine wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe.
Katika ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko, amekuwa mfano mwema wa utangamano na sioni uwezekano wa kupatikana mwingine kama yeye katika miaka mingi ijayo."
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ametangaza siku tatu
za maombolezi, kufuatia kifo cha mzee Nelsomn Mandela, akisema kua
Afrika na dunia nzima kwa ujumla imempoteza shujaa mkubwa sana katika
karne ya 20 na 21.
Kikwete alisema kupitia taarifa kwa vyombo vya
habari kua Mandela ni kiongozi wa kipekee na mtu aliyeenziwa sana na
dunia nzima pamoja na watu wa Afrika Kusini baada ya kupigania sana
demokrasia nchini Afrika KusinKikwete alisema mfano wa Mandela unapaswa kuigwa na watu wote duniani .
Kwa upande wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesema kuwa Mandela alikuwa mfano mzuri wa umuhimu wa kuwa na matumaini na kuwataka watu kuwa na uelewa wa kuwasamehe bila masharti wale wote wanaotukuosea.
Naye Rais wa Rwanda Paul Kagame,amesema kua Mandela ataendelea kuishi kwenye mioyo ya wengi wetu.
Naye Rais mstaafu Daniel Moi ambaye alikuwa madarakani wakati Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amempongeza Mandela kwa kuhakikisha utulivu wa kisiasa barani Afrika na kuwa mfano bora kwa viongozi wengine.
Naye Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema kuwa Mzee Mandela, pamoja na washirika wake, Albert Luthuli, Walter Sisulu, Govan Mbeki, Oliver Thambo na wengine wengi,walijitolea maisha yao kuleta demokrasia nchini Afrika Kusini.
Walifanya kila walichoweza kuhakikisha kwa wanawakomboa watu wa taifa lao.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Museveni amesema ni jukumu la vijana sasa kuiga mfano wa Mandela kuhakikisha kuwa Afrika inalindwa dhidi ya ukoloni mambo leo na kutengwa.
0 comments:
Chapisha Maoni