JESHI la Polisi mkoani Singida limewauwa watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP, Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo limetokea desemba tisa mwaka huu saa 12:00 jioni, huko katika
kijiji cha Manga nje kidogo ya mji wa Singida.
Amesema
watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki moja ya
kijeshi aina ya SMG, walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya
uhalifu.
Kamanda
Kamwela, amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi kwenye chumba cha
mochwari katika hospitali ya mkoa, majina na makazi yao bado
hayajajulikana.
Akifafanua,
amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia jeshi la polisi
na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.
“Baada
ya polisi kufika kijijini hapo watu hao walistuka kuwa wanafuatilwa na
askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha Uhamaka kwa
kutumia pikipiki yenye namba za usajili T. 634 BTW aina ya Sanlag yenye
rangi nyeusi”,amesema Kamwela.
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia waliamua kutelekeza pikipiki yao hiyo na kuanza kukimbilia porini kwa miguu.
“Hali
ilipokuwa ngumu zaidi, walianza kuwarushia polisi risasi, hivyo polisi
nao ikwabidi kujibu mapigo. Katika majibizao hayo ya risasi, majambazi
mawili yaliweza kujeruhiwa huku mmoja akifanikiwa kutoroka”
Amesema
majambazi hayo yaliyojeruhiwa yalifariki dunia wakati yanakimbizwa
katika hospitali ya mkoa kwa matibabu,lakini yakafia njiani.
Amesema
katika eneo la tukio, ilipatikana bunduki moja aina ya SMG yenye namba
34555 ikiwa na risasi saba kwenye magazine. Pia pikipiki iliyokuwa
iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana.
Kamwela
alitoa wito kwamba wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua
watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya
uhalifu.
0 comments:
Chapisha Maoni