Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kiongozi wa
zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela yuko katika hali mbaya sana
hospitalini, lakini madaktari wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha
hali yake inaimarika.
Ni taifa lililoko katika sala, raia wengi wa Afrika wanaendelea kutumaini kuwa Nelson Mandela anapata nafuu ya haraka. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini amekuwa hospitalini tangu tarehe 8 Juni, akitibiwa kufuatia maambukizi ya mapafu, lakini madaktari wanasema afya ya Mandela, ambaye anajulikana kama Madiba, inazidi kuwa mbaya.
Wananchi wa Afrika Kusini wanaelekea kazini asubuhi ya leo wakiwa na simanzi huku wakisubiri habari kuhusu afya ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye madaktari wanasema yuko mahututi.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zilisema Jumapili
jioni kuwa Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila
wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni.Ni taifa lililoko katika sala, raia wengi wa Afrika wanaendelea kutumaini kuwa Nelson Mandela anapata nafuu ya haraka. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini amekuwa hospitalini tangu tarehe 8 Juni, akitibiwa kufuatia maambukizi ya mapafu, lakini madaktari wanasema afya ya Mandela, ambaye anajulikana kama Madiba, inazidi kuwa mbaya.
Wananchi wa Afrika Kusini wanaelekea kazini asubuhi ya leo wakiwa na simanzi huku wakisubiri habari kuhusu afya ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye madaktari wanasema yuko mahututi.
Mandela ambye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka 94,alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.
Rais Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu.
Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.
Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu wanaomtibu.
Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.
Afya yake kutoathiri ziara ya Obama
Zuma amesema yeye na makamu wa rais wa chama cha Africa National Congress, ANC, Cyril Ramaphosa walimtembelea Mandela usiku wa kuamkia leo. Lakini amekataa kutoa maelezo zaidi kuhusu afya ya Mandela, zaidi ya kusema kuwa yuko katika hali mbaya sana. Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kufanya ziara nchini Afrika Kusini wiki hii, lakini Zuma amesema kuwa kudorora kwa afya ya Mandela hakutaathiri ziara hiyo.
Kudorora kwa afya ya Mandela wikendi hii, ikiwa ni wiki mbili tangu alipolazwa akiwa katika hali mbaya lakini imara, kumeibadili hali kutoka kwenye kumuombea kupona haraka hadi kwenye kuanza maandalizi ya kumuaga. "Kama ni wakati wa yeye kuondoka, anaweza kuondoka, namuombea kwa Mungu ampokee vyema," alisema Petunia Mafuyeka, ambaye ni Nesi wakati akielekea kazini mjini Johannesburg.
Baadhi wataka aachwe apumzike
Kulikuwepo na wasiwasi miongoni mwa umma kuhusu jitihada za madaktari kurefusha maisha ya rais huyo wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, ambaye ni mmoja wa watu maarufu zaidi duniani katika karne ya 20. "Nina wasiwasi wanajaribu kumuweka hai, nadhani wanapaswa kumuacha aondoke," alisema Doris Lekakala, Meneja madai. Ameshakuwa mzee, waache tu mambo yachukuwe mkondo wake. Anapaswa kupumzika."
Tangu alipostaafu mwaka 1999 baada ya muhula mmoja kama rais, Mandela amejiweka mbali na siasa, katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, na endapo atafariki kunatizamiwa kuwa na athari ndogo kisiasa. Mara yake ya mwisho kuonekana hadharani ilikuwa Julai mwaka 2010 wakati wa mashindano ya kombe la dunia.
Umma ulipata kumuona mara ya mwisho katika picha ya video iliyotangazwa na televisheni ya taifa mwezi April, wakati rais Zuma na viongozi wengine waandamizi wa ANC walipomtembelea nyumbani kwake. Wakati huo, chama cha ANC kiliuhakikishia umma kuwa Mandela yuko katika hali nzuri, ingawa picha hiyo ya video ilionyesha mtu mzee aliedhoofu, akiwa amekaa katika kiti bila hata kutikisika.
Wafanyakazi wa Posta wakiyapita magari ya vyombo vya habari yaliyoegeshwa nje ya hospitali alikolazwa Mandela. Hiyo ndiyo hali ilivyo katika tukio zima la kuuguliwa na mpendwa wetu mzee Mandela, tusikata tamaa bali tuendelee kumwombea na huku tukisema mapenzi ya Mungu yatimizwe
0 comments:
Chapisha Maoni