Alhamisi, 18 Aprili 2013

KAKOBE ANAPELEKA INJILI NCHINI CANADA!!!

Hii ni historia katika nchi ya Tanzania, mtanzania anapenya hadi katika mataifa makubwa kupeleka habari njema za Injili ya Yesu Kristo, kwa hakika kiroho tunasema sifa na utukufu ni kwa Bwana Yesu, lakini kimwili tunasema Kakobe anaiinua Tanzania kwa namna ya pekee sana hapo jijini Toronto na Canada kwa ujumla. nadhani ufike wakati sasa inapotokea safari kama hizi za Injili, ingependeza watu kama akina Askofu Kakobe kuambatana na ujumbe wa serikali
Tanzania sio tu kwamba imejaliwa ardhi nzuri, au madini, bali pia Tanzania imejaliwa vipawa vya kiroho, sio jambo dogo kwa mzungu na wasomi kumkubali mtu kiasi hiki cha akina kakobe, na jaribu kuwaza hata Don Moen atashiriki katika mkutano huo wa kakobe huko Canada, Don moen sio mtu wa kwenda popote tu anapoitwa, ni baba wa imani na mtu wa kiroho wa siku nyingi, mwimbaji wa nyimbo za sifa na kuabudu, na ndani sifa na kuabudu Mungu umfunulia mengi katika huduma yake.

2 comments:

  1. kazi yenu njema, tuzidi kuomba kwa ajili ya milango mikubwa ya injili ulimwenguni.

    JibuFuta
  2. Imenifurahisha zaidi baada ya kusikia kuwa atahubiri kwa KISWAHILI, nadhani huu ni wakati mwafaka kwa Watanzania wote kumpa support. Yeye akienda huko ataitangaza nchi yetu ya Tanzania pia,

    JibuFuta

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595