Kumetokea vurugu kubwa mjini Mtwara, vurugu ambazo zimesababiswha na wananchi na wakazi wa Mtwara, vurugu hizi zilianza tu mara baada ya waziri wa nishati na madini kusoma bajeti ya wizara hiyo, na katika bajeti ya wizara hiyo, serikali ilionyesha mpango wake wa kujenga bomba la kusafirishia gesi kutoka mikoa hiyo ya kusini hadi Dar es salaam. wananchi wanampinga mpango huo wa serikali, wanataka mpango huo usitishwe ns kinyume chake kila kitu kuhusiana na gesi kibaki mkoani Mtwara
kabla ya kutokea vurugu hizi, siku mbili kabla ya tukio, kulionekana kuna kampeni kubwa ya kusambazwa kwa vipeperushi vilivyokuwa vikiwataka wananchi kufanya fujo na kupinga uamuzi wa serikali utakao tolewa, kuna mambo mengi ya kujiuliza katika mazingira haya,
jambo la kwanza, ni nani anayechapisha vipeperushi hivyo na kuvisambaza? kwanini asichukuliwe hatua kali za kisheria na kinidhamu? je hii gesi ni mali ya wakazi wa Mtwara au ni rasilimali za Taifa chini ya usimamizi wa serikali? je kila mkoa sasa uangalie ilichonacho na kukifanya kuwa mali yao? wale wenye samaki au madini katika mikoa yao, je nawao wafanyeje ikiwa mfano ndio huu?
sasa tazama, gesi imegeuka na kuwa damu!! tayari watu kadhaa wamekwisha fariki kutokana na vurugu hizi, hao ni pamoja na askari wetu wa JWTZ waliokuwa wakielekea eneo la tukio kwa lengo la kutuliza ghasia, na raia pia wameripotia kupoteza maisha!! na wengine kujeruhiwa vibaya!! hii maana yake ni nini? je kuna mkono wa kisiasa katika vurugu hizi kwa lengo la kutafuta kuwaonyesha wananchi wa Mtwara ubaya wa serikali iliyopo madarakani? je hiyo ndiyo demokrasia?
sauti ya kanisa, inalaani na kupinga vitendo vya vurugu zilizo tokea Mtwara, kwakuwa wayafanyao hawajakaa chini na kutafakali kwa kina, lakini pia ndani mwao wamejaa ubinafsi na kudhani kilichoko Mtwara ni chao na sio cha Tanzania
Tunamwomba Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, sawa na alichotamka kwenye hotuba yake jana, kitendeke, vurugu hizi zinafanywa na watu wachache sana na wala sio wananchi wote wa Mtwara, ndio maana watu wanakimbia makazi yao kwa kuepuka vurugu hizo, polisi na jeshi fanyeni kazi yenu ipasavyo bila kuogopa chochote, kwakuwa Rais amewapeni agizo la kufanya
Vurugu hizi zimetokea siku chache baada ya Wizara ya Nishati na Madini kusema kuwa bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam na leo hii Wananchi wa Mtwara wacharuka na kuanzisha vurugu!
Tukio hili liliendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa Bungeni.
Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutukia Mtwara.
Fullshangweblog imewasiliana kwa njia ya simu usiku huu na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara Kamanda ACP Linus Sinzumwa, hata hivyo ACP Sinzumwa alisema yuko kwenye kikao hataweza kuongea chochote na kukata simu.
Tukio hili liliendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa Bungeni.
Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutukia Mtwara.
Fullshangweblog imewasiliana kwa njia ya simu usiku huu na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara Kamanda ACP Linus Sinzumwa, hata hivyo ACP Sinzumwa alisema yuko kwenye kikao hataweza kuongea chochote na kukata simu.