Jumatano, 15 Mei 2013
RAIS WA NIGERIA ATANGAZA HALI YA HATARI
Wanajeshi nchini Nigeria wameenezwa katika majimbo matatu ya kaskazini ambako Rais Goodluck Jonathan ametangaza hali ya dharura kujibu harakati za waasi wa ki-Islam.
Magazeti nchini Nigeria yanaripoti kuwa kiasi cha wanajeshi 2,000 wakisaidiwa na ndege za kivita wamewasili katika jimbo la Borno huku mashahidi wakiripoti mtiririko wa wanajeshi katika majimbo jirani ya Yobe na Adamawa.
Rais Jonathan alisema Jumanne kwamba waasi wameteka maeneo ya jimbo la Borno na aliagiza idara za usalama kutumia hatua zote muhimu kusitisha kile alichokiita uasi katika eneo la kaskazini.
Kundi la ki-Islam lenye msimamo mkali la Boko Haram lenye makao yake Borno linapigana na serikali tangu mwaka 2009. Kiongozi wa kundi hilo alitoa mkanda wa video wiki hii akidai kuhusika kwa mashambulizi ya karibuni katika miji ya Baga na Bama na alisema kundi hilo litaanza kuwateka nyara watu kama sehemu ya mkakati wake.
Makundi ya haki za binadamu yanaikosoa serikali ya Nigeria kwa kutumia nguvu kupita kiasi na kuwauwa raia katika juhudi zake za kusitisha ghasia.
Wakazi wa Baga wanasema majeshi ya usalama yalichoma maelfu ya nyumba baada ya mwanajeshi mmoja kuuwawa na kundi la Boko Haram. Jeshi linakanusha shutuma hizo.
Rais Jonathan alisema Jumanne wanajeshi wapya waliowekwa huko wataruhusiwa kuwakamata watu, kudhibiti jengo lolote lililotumika kwa sababu za ugaidi na kuwaweka kizuizini kwa muda watu ambao wanatumia silaha kinyume cha sheria.
Posted By:
Unknown
On 10:54
In
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595