Ijumaa, 26 Aprili 2013

MBARONI KWA KUFANYA MAPENZI NA KUKU, MWENYE KUKU APIGA KELELE AKIOMBA MSAADA

HAYA NI MAAJABU AU NIDALILI ZA MWISHO WA DUNIA?

Kabla ya kuanza kumshughulikia mtuhumiwa ni vema kwanza kuangalia kile alichokitenda na kukilinganisha na kawaida ya binadamu, kwasababu wakati mwingine unaweza kudhani ni yule mtu, kumbe kuna nguvu au roho nyingine ndani ya yule mtu inayomtuma kufanya kitendo kile, kwa mfano, hivi unawezaje kumshika kuku kama huyo hapo na kumnajisi? unawezaje kumwona kuku na kisha ukaanza kumtamani kimapenzi? jamani kuku!! hayo ni maajabu yaliyotokea huko mjini Musoma mkoani Mara. soma kisa hiki

MWANAMUME mmoja mkazi wa Kata ya Kigera Manispaa ya Musoma, Yusufu Bakari (28), anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na kuku. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma alisema tukio hilo lisilo la kistaarabu, lilitokea juzi saa tatu asubuhi.

Mwakyoma alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alimchukua kuku wa mama mwenye nyumba wake, mahala anapoishi na kuingia naye ndani na hivyo kutimiza azma yake.

Kamanda Mwakyoma alisema, wakati akifanya kitendo hicho, mama mwenye kuku alipiga kelele, hatua iliyowezesha majirani kuzingira nyumba hiyo na kumkamata mtuhumiwa.

Katika tukio jingine, Mwakyoma alisema mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Elizabethi Bureko (26) mkazi wa Kata ya Nyamatare, anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumchoma kwa moto mtoto wa miaka (8), Robhi Marwa sehemu zake za siri na kumsababishia maumivu makali.

Chanzo cha kuchomwa moto mtoto huyo ni pale alipokutwa na mama huyo akimnywesha uji mtoto wake wa miaka 2, huku akiendelea kulia na kudai mlezi alikuwa akinywa uji wa mtoto ndipo alipochukua kibatari na kuanza kumchoma.

Kamanda Mwakyoma alidai baada ya majirani kupata taarifa za tukio hilo, walimfuata mtuhumiwa na kuanza kumshambulia kwa kipigo.

“Matukio kama haya mtu inatokea anayafanya bila kuchukua muda wa kuishughulisha akili kabla ya kufanya, maana kitendo cha kumchoma mtoto wa miaka 8, ni kitendo cha kinyama,” alisema.

0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595