Jumatano, 24 Aprili 2013

MAASKOFU WALIOTEKWA SYRIA SASA WAACHIWA HURU


Metropolitan Paul Yazigi kushoto, na Mar Gregorious Yohanna Ibrahim. ©Orthodox Church America
Maaskofu wa Syria wa kanisa la Orthodox na Greek Orthodox, Mar Gregorian Ibrahim na Paul Yazigi wameachiwa huru bila kudhuriwa, mara baada ya kuwa mateka wa waasi  tokea siku ya jumatatu.
Tunajua dhahiri umuhimu wa maaskofu hawa kwa wakristo wa Syria hapa Aleppo, wanawatia sana moyo na kuwahamasisha wabaki kwenye taifa lao, anasema Askofu Munib Younan wa kanisa la kiinjili la kilutheri nchini Jordan na kwenye taifa takatifu, kwa mujibu wa huduma ya kikristo ya SAT-7.
Gari la maaskofu hao lilisimamishwa Jumatatu (22 Aprili) wakati ambapo walikuwa wakitokea kwenye majadiliano kuhusu kuachiwa kwa wakristo waliotekwa na waasi wa Syria, ambapo dereva wao alipigwa risasi na kisha wao kutekwa.
Mabaki ya kanisa la Mtakatifu Mary lililoko Homs, Syria ©Barnabas Fund
Awali akizungumzia utekaji huo, Papa Francis alielezwa kusikitishwa na hali ilivyo nchini Syria, ambapo aliomba amani ipatikane katika nchi hiyo ambayo zaidi ya wananchi milioni moja wameshakimbilia nchi jirani ili kujinusuru, huku wengine zaidi ya 75,000 wakifariku kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, ambapo waasi wanataka kuondoa utawala rais Bashar al-Assad.

0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595