Siku ya jumapili, ni siku ambayo
Wakristo wanakwenda kanisani kumwomba Mungu na kumwabudu, watu wanaketi pamoja
na kuimba nyimbo za sifa na kumwabudu Mungu, kisha kulisikia Neno la Mungu na
kumwomba mwenyezi Mungu juu ya mahitaji yao, siku hii ya jumapili ujulikana pia
kama ya siku ya Bwana, kwa wengi ni siku ya kutokufanya kazi na inatengwa kama
siku ya kumpa Mungu utukufu kwa yote aliyoyatenda kwa wiki nzima, kama maneno
ya Mungu yanavyosema kwamba, mtu hataishi
kwa mkate tu, bali kwa kila neno litokalo kwa Bwana” uzima wa mtu upo katika
maeneo mawili, lakwanza ni mwili na eneo la pili ni roho, mwili unategemea kula
ndipo uweze kuishi, na ukiwa na mgonjwa na akafikia hatua ya kutokula chakula,
ndugu wanaanza kuwa na mashaka juu ya uhai wa ndugu yao, lakini kama atakuwa
anakula, kwa sehemu uleta matumaini ya kuishi. Eneo la pili ni uzima wa roho,
uzima au afya ya mcha Mungu utegemeana na jinsi anavyokula na Neno la Mungu na
kulitenda, kwahiyo tukimwona mtu anakosa ibada tutambue amekosa chakula, na
kama amekosa chakula ni hakika nguvu zake za kiroho pia zimepungua, na
akiendelea kutoshiriki katika ibada kwa muda mrefu, yule mtu anakufa kiroho,
kwani utaweza kumwona akiyafanya mambo yaliyo kinyume na Neno la Mungu
Ndivyo inavyoonekana kwa waumini
hawa wa kanisa la AMANI CHRISTIAN CENTRE-HEMA YA FARAJA, wao wametambua faida
ya Neno la Mungu na ndio maana wanamtafuta Bwana Yesu kwa gharama yoyote bila
kuangalia mazingira, kanisa la Amani Christian Centre, lipo maeneo ya Bunju B,
eneo la bunju lipo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, ni pembezoni kabisa mwa
barabara iendayo Bagamoyo, kama unatokea Mwenge, utavuka kwanza Tegeta na kasha
Boko, baada ya Boko ndipo utakapo yafikia maeneo ya Bunju.
Mchungaji wa kanisa la Amani Christian
Centre akihubiri ujumbe kutoka kitabu
cha LUKA 1:26-35, mahubiri hayo yalikuwa yakizungumza juu ya ondoleo la dhambi,
uwezo wa Yesu wa kumbadirisha mtu na kumjalia neema ya kushinda dhambi
Lakini pamoja na mambo mengine
niliyoyaona, ninatamani uangalie picha za kanisa la Amani lililoko bunju na
kama unaweza kufanya kitu chochote au kuwa na mzigo wowote, basin i vema
ukafanya hivyo na utabarikiwa pia, jumapili ya tarehe 28-04-2013, wakati ibada
inaendelea mahali hapa, mvua ilianza kunyesha, Mchungaji alisema ndugu zangu,
bati zilizo salia kukamilisha hapa juu ni bati 36, tuzidi kumwomba Mungu
atufungulie mlango wa mabati hayo
Je mpendwa na msomaji wa sauti ya
kanisa, unadhani unaweza kufanya nini kwaajili ya kanisa la Amani au kanisa
lolote lenye hali kama hii? Je unawaonaje wakristo na ndugu zako wa hapo bunju
wanavyo abudia mahali pa jinsi hii? Nakuachia wewe mwenyewe uweze kutafakari
jumapili hii ya leo
Kila neno au tendo mfanyalo,
fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu
0 comments:
Chapisha Maoni