Kwa Taarifa zilizopatikana punde, ni kuwa yule mwimbaji maarufu na
mkongwe wa muziki wa Mwambao FATMA BINTI BARAKA alimaharufu kama Bi
Kidude amefariki hii leo...
Taarifa hizo pia zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa Bi Kidude! Chanzo cha umauti ni maradhi yatokanayo na uzee!
Bi Kidude amefariki ktk hospitali ya Hindu Mandal... Atakumbukwa kwa
umahili wake ktk nyimbo za Taarabu ndani na nje ya nchi...alama ya
Utamaduni wa Mzanzibar ktk matamasha ya muziki kama ZIF na Sauti za
Busara.
...itakumbukwa hivi karibu Bi Kidude na baadhi ya Wanamuziki nguli kama
Muhidin Ngurumo walitunukiwa Nishani ya heshima ktk mambo ya muziki pale
Ikulu....
---
Wasifu Wake:
Mwanamuziki
mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude
amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar, sehemu
alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake
Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha
Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa
Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha
miaka 102.
Katika
mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya
sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es
Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940
alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa
nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi
Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na
katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba
katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni.
Jumatano, 17 Aprili 2013
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595
0 comments:
Chapisha Maoni