Jeshi la polisi wilaya ya Kinondoni lawatia mbaroni machangudoa zaidi ya 51 wanajiuza usiku.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela akionyesha moja ya silaha walioyofanikiwa kuikamata katika Operesheni hiyo.
Na.Mo Blog Team
Katika
operesheni za kupambana na uhalifu zinazoendelea katika mkoa wa
kipolisi wa Kinondoni Jeshi la polisi likishirikiana na askari mgambo na
ulinzi shirikishi kutoka manispaa ya kinondoni limefanikiwa kuwakamata
jumla ya wanawake 51 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya kujiuza
kimwili hadharani.
Wanawake
hao wamekamatwa katika maeneo ya Msasani Mikoroshini, Mwananyamala,
Kinondoni Barabara ya Tunisia, Sinza Corner Bar na maisha Club.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles
Kenyela amesema wanawake hao pia hutumika kuwapora mali wanaume kwa
kuwawekea madawa ya kulevya katika vinywaji, vyakula na hata katika
miili yao na pia kushirikiana na wahalifu wakiwemo majambazi katika
kufanya matukio ya aina mbalimbali ya kihalifu.
Wakati
huohuo jeshi hilo limefanikiwa kukamata mtandao wa matapeli hatari na
pia kuwakamata watuhumiwa wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa
na silaha bastola na mirungi.
0 comments:
Chapisha Maoni